top of page

Miradi

Katika kuhakikisha jamii inawezeshwa kikamilifu, TALISDA Foundation inafanya kazi na wadau wanaojitolea katika sehemu mbalimbali. Tunajivunia katika kufikia maeneo mbalimbali kama ya kijamii mazingira, kiuchumi na kwakiwango kizuri,na

maswala mengine mtambuka kama vile masula ya ukimwi, jinsia na watu wanaoishi na ulemau.

Pamoja Tuwalee
Mradi huu unafadhiliwa na wamanekani (USAID) ili kuwezesha familia zilizopo katika mazingira hatarishi. Tunakusanya taarifa kuhusu watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na kuwaletea  kuweza kupata mahitaji yao kutoka serikalini, (tunapambana wapate matibabu bure na huduma ya chakula shuleni). Zaidi tunajikita kwenye wajitolea wa jamii kama vile vikundi vya kuweka na kukopa (LIMCA) na kamati za watoto walio katika mazingira hatarishi kwa wapatia mafunzo na usimamizi. Katika shule, tunatekeleza mradi kwa kutumia klabu za haki za watoto kuwaelimisha kuhusu kupaza sauti zao, kupunguza ukatili mashuleni na kupambana na utoro.
Lengo kubwa ni kuongeza viwango vya maisha vya jamii na kujitegemea kupitia uimarishaji uchumi, elimu ya stadi za maisha, na uwezeshwaji  na kwa kuongeza, kuwaweka watoto wetu katika afya na usalama.
more information
WEKEZA

Wekeza -wekesha ustawi, endeleza kiwango cha Elimu kuzuia Ajira kwa watoto. Mradi huu umeundwa kutoa huduma kwa watoto wanaofanya kazi au walio katika hatari ya kuingia kwenye ajira, vijana wasioajiriwa, na familia zao ili kupunguza manikio ya ajira kwa watoto na kujikita kwenye kilimo na shughuli za nyumbani.

Kwa upande mwingine, shughuli za mradi zinahusisha elimu ya moja kwa moja, stadi za maisha, ajira ya vijana na msaada wa kiufundi. Pia tunazihusisha mamlaka husika, kujumuisha masuala ya ajira kwa watoto kwenye mipango nasera taifa za elimu, kilimo na nyingine za ulinzi wa mtoto.

Tunaunga kubadilisha mitazamo kwenye jamii lengewa Kuhusiana na ajira kwa watoto kwa kukuza uelewa juu ya madhara ya utumukishwaji wa watoto katika umri mdogo.

more information
Mradi wa Elimu Mombo

TALISDA inatekeleza mradi huu Kwakushiriki ana na Foundation for Civil Society (FCS) Kusaidia jamii Kupambana na tatizo la Uhudhuriaji mdogo wa watoto shuleni. Tumezijikia shule 32 za msingi hapa mombo, na Kuwapa elimu watu wa baralza la elimu la katk, ambao wanayo madaraka juu ya matatizo juu ya elimu mombo, Kama vyoo vya shule, ubao, upungugu wa madawati, vyumba vya kusomea, chakula. leng. nikuinucoa Kiwango cha elimu na kuwa Janya watoto wapende shule. Natuna ihimiza jamii juu ya Umuhimu wa elimu ya msingie. Na hii inaongeza mahudusio mazeuri kwa walimu na wanajunzi. Inapunguza asilimia ya atoso kwa kiwango cha 2%.

more information
Shule ya Chekechea

Kuanzia mwaka 2011, tunajivunia kuianzisha shule nzuri ya chekechea, kwa kiwango cha watoto 30, wenye miaka tatu na miaka sita wanao gawanyika katika madarasa mawili. Tunaona kuwa elimu ni ufunguo wa maisha na ni njia pekee ya maisha bora. tunao walimu bora na makini katika kuwafundisha watoto vizuri sana ili siku watakapo jiunga na shule ya serikali au watu binafsi wawe wamepata mwanzo mzuri. Tuna lenga kuwa fundisha watoto masomo ya kusoma, kuandika na hisabati. Na pia kujifunza kuimba (Kiswahili na Kingereza). Pia tunayo michezo mbalimbali kwa watoto na  tunawapatia watoto chakula kwa muda wa asubuhi.

 
Udereva

Tangu 2011, tumetoa piahuduma ya shule ya udereva kama sehemu ya programu yetu ya maendeleo ya vijana. Mpango wetu ni kuwezesha jamii kwa wingi na kuongeza nafasi za ajira kwa vijana kwa kuwapatia leseni rasmi zaudereva. Masomo yetu ya mwezi mmoja yanahusisha mafunzo ya nadgaria na vitendo ili kuweza kuwaa-ndaa vizuri. Kupitia kampeni tumeshawafikia watu zaidi ya mia nane (800) ambapo ni muhimu chuo pekee cha udereva Korogwe mji.

 

bottom of page