top of page

Habari

01/04/2016 Pamoja tuwalee:  Upimaji wa hali ya lishe na hali ya mambukizi ya virusi ya ukimwi

 

Kati ya tarehe 29th ,February  mpaka  16th March ,tulikuwa na mikusanyiko mingi hasa katika shule za Msingi Korogwe mji .Utaratibu ukiwa chini ya pamoja tuwalee  Kupitia Talisda foundation. Kulikuwa na vikosi vilivyo ambatana nao, watu wa kitengo cha afya(Wauguzi,Madacktari ,Nawatoa ushauri nasaha) wakiambatana na watu wengine sita kutoka Talisda Foundation  ambao wameweza kusimamia zaidi ya watu 7029.Tunafurahi kutangaza kwamba nambari ya waoto wasio na maambukizi ya HIV yamekuwa chini ya mtazamo kwa asilimia (0.5%). Kwa kusikitisha jumla ya upimwaji lishe kwa watoto hali ilikuwa sio nzuri  takribani jumla ya watoto 730 walikuwa na NJANO na NYEKUNDU hii imesababisha watoto wengi kuwa na uzito wa chini na afya duni.Pia tulifanikiwa kufikia watoto waliokokatika mazingira hatarishi takribani 1900.Watoto walio katika mazingira hatarishi pamoja na walio pata maambukizi ya (HIV)wote kwa ujumla walipata  ushauri nasaha kuhusu afya na  ujuzi wa huduma ya kwanza .Mengine zaidi  watoto wenye lishe duni pamoja na  wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi  walipewa rufaa ili waweze kutembelea vituo vyao husika kwa matibabu na msaada zaidi.Wazazi walio fika pale walikuwa makini katika kusikiliza  na kuangalia zoezi  la upimwaji lishe kwaumakini.Tunaamini taarifa hii itakuwa na mabadiliko makubwa hasa katika upimaji lishe na hali ya maambukizi ya ukimwi ndani ya Korogwe mjid.

18/01/2016 Recent Wekeza Follow-Up
 

Wiki iliopita, mwezi wa pili targhe 16 hadi 18, ilikuwa ni muda wa kusafiri Korogwe nzima Kuangalia matokeo ya mkakati wa WEKEZA. Katika siku tatu tulitembelea vijiji kumi. Timu ilijumuisha wafanyakazi wa TALISDA Mwanamvua Mwalimu na Joseph shemzigwa, wote wakiwa ni wahusika wa WEKEZA na mkurungenzi wety Joseph Noya. Pia tulikuwa na heshima kubwa kuambatana na Mama Anna Mgina (maendeleo ya jamii), Dickson Mgaya (ustaui wa jamii) na James Lymo (Elimu) wajumbe muhimu wa halmashauri ya mji Korogwe. Kuhakikisha muendeleo wa mradi, tulitathimini maendeleo kwenya maeneo ya elimu na stadi za maisha. Kwa upande mwingine, tuliongea na wakuu wa shule na walimu wa shule shiriki, pia viongozi wa VICOBA na vikundi vidogo vya fadha. Ingansa bado kuna changamoto za kushughulikia tulifurahi kukuta mikakati mingi imefanikiwa. Madarasa yamekarabatiwa ili kuweka mazingira mazuri ay kufundisha na kujifunza na yanarufia sana.

Vivunia asali na tingatinga vimenunuliwa ili kuongeza kipato. Kahibia asilimia 90 (90%) ya malengo imefikiwa. Kwa hiyo, Karika kila kitu tumefanikiwa kutusheleza na kuchochea matokeo.

Hatua ya Mahojiano

 

Mwaka mpya ulianza kwa matukio: Kuanza kwa awamu mpya ya mradi mkubwa, Pamoja Tuwalee, ambapo utafutaji wa wafanyakazi ulifanyika kwa matangazo kwa umma. Tulipokea maombi kutoka kwa waombaji 23 kwa ajili ya nafasi mbalimbali kwenye ngazi mbalimblai kama vile Mratibu wa mradi, Afisa Ufuatiliaji na Tathmini Mhasibu wa mradi, Afisa mhimarishaji uchumi na waelimishaji jamii-katika usahili waombaji walijitambuwa uelewa wao juu ya kompyuta, elimu yao umahiri wao katika maswala ya watoto na ufanyaji kazi wa pamoja na umahili wao katika kuongea na kuandika kwa lugha ya kiswahili na kingereza.

TAARIFA KABLA YA KUFUNGA OFISI KWA AJILI YA LIKIZO YA MWISHO WA MWAKA 

 

Kama ilivyo kila mwaka krismasi huja wakati watu wakiwa na shughuli nyingi za kufunga mwaka Kazi hizi zote zilitakiwa ziishe tarehe 23.12.2014 na hii ndiyo tarehe ya kufunga ofisi mpaka tarehe  05.01.2015.
ikiwa ni pamoja na kufanya maandalizi kwa ajili ya sikikuu. Ghafla mwezi wa 12 umefika sisi, wafanyakazi wa TALISDA Foundation kama walivyo watu wengine , tulikuwa na kazi nyingi kwa sababu mwaka ulikuwa unaisha. Tulifanya mahesabu ya pesa za shirika zilizotumika kwa mwaka ikwa ni pamoja na kutoa taarifa ya matumizi ya pesa hizo.
Siku ya mwisho tulisherekea kidogo kwa pamoja hapa ofisini. 

 

Kwanza mkurugenzi a shirika letu bwana Adolph Noya, Samweli Shemzigwa (mwenye kiti TALISDA), na wafanyakazi  7 tulienda kutembelea vijiji viwili. Tulitembelea vikundi vya LIMCA viwili. Kijiji cha kwanza (Kwamsisi) wanawake wengi walitupokea na  nyimbo nzuri sana. Tulikaa pamoja kwenye kivuli na mfanyakazi mmoja alikuwa MC. Halafu utambulisho kwa ufupi ulifanyika kisha tukapata maelezo kuhusu shuguli za LIMCA. Nini walifanya mwezi wa 12 na wanataka kuendelea vipi. Halafu tuliangalia kibanda cha kuku, walichotengeneza. Pia sisi tuliwaambia kuhusu shughuli yetu kidogo. Tumefurahi kuona wanaendelea vizuri. 

Tuliendelea na safari yetu kwenda Kwakombo. Huko tulikutana na kikundi cha LIMCA kimetengeneza kausho (Solar Dryer). Tuliona wanatunza vizuri na muda tumefika walikuwa wanakausha mboga kama nyanya na mboga za majani ndani watu wote walifurahi sana hasa vijana wakujitolea wa Ujerumani. Vijana walikausha matunda ndani ya Solar Dryer ya TALISDA ofisi. Sasa wanaweza kuangalia uwezekano wa kukausha mboga ndani Solar Dyer pia. wanakikundi cha LIMCA walituambia pia kuhusu shughuli zao na sisi tuliwaambia kuhusu shughuli yetu. Ni kitu kizuri kuona kwa macho watu wanavyoshughulika kwenye kikindi cha LIMCA. Kikundi kinafanya kazi vizuri.

 

Halafu tulirudi ofisini kwa ajili ya kumaliza mwaka pamoja.

 

Wafanya kazi 21 walikaa ndani ya chumba kimoja. Wote walifurahi kusikiliza taarifa za mwaka. mwenyekiti na na mkurugenzi walieleza. Wow! TALISDA imeshinda shuguli nyingi kweli. Tumefurahi kukumbuka tumeshinda nini, lakini pia tumeongea kuhusu changamoto zilizopita na ratiba kwa mwaka kesho.
 Pia tuliwasha mishumaa minne ya “Adventskranz“. Hii ni desturi iliyoletwa na vijana wakujitolea wa Ujerumani. Haya ni mashada ambayo watu wa Ujerumani wanatengeneza wiki nne kabla ya krismasi na kila jumapili wanawasha mshumaa mmoja wanaendelea kuwasha mwingine kadiri jumapili zinavyoongezeka kwa kuwasha na mingine iliyokwisha washwa na mwisho mishumaa minne inawaka. Kila jumatatu wafanyakazi TALISDA Foundation walipata zawadi moja halafu kuwasha mishumaa. Leo wamepata matunda yaliyokaushwa na extenion cabel kwaajili ya ofisi. 

 

Uliwadia wasaa wa furaha zaidi ambapo mkurugenzi na mwenyekiti walitangaza wafanyakazi wa mwaka (employees of the year). Izack Mbilinyi na Yona Godwin walipata vyeti. Hongera! Halafu Elisha Martine, Lilian Mdoe, Seif Mohamed, Dativa Sweetbert na Vicent Njama walipata vyeti kwa kujolitolea. Hongera pia!

 

Kisha tulikula chakula kitamu cha mwisho wa mwaka kwa pamoja. Wote walifurahi kuenda likizo kwa kusherekea krismasi na mwaka mpya.

 

Kwa hivyo:

Heri ya krismasi na mwaka mpya!

Tutaonana tena tarehe 5.01.2015

TALISDA MEETS NRCF - TALISDA IMETEMBELEA NRCF

 

Tarehe 29-30.10.2014

Washiriki: wafanyakazi 8 wa Talisda, wafanyakazi  3 wa NRCF 

 

Saa 3.00 Asubuhi wafanyakazi wanne waliondoka TALISDA ofisini kwenda kukutana na wafanzakazi wa NRCF (New Rural Children Foundation). NRCF ni shirika lisilo la kiserikali lililoko Korogwe. Linafanya kazi kuhusu mambo mengi. Lakini tulienda kwa sababu ya kujifunza mambo kuhusu mtambo wa biogesi. Shirika hilo lina ubia na Tanzanian Domestic Biogas Program.

 

Tulipofika NRFC tulijifunza vipi mtambo wa biogesi unafanya kazi. Hapo chini ni maelezo mafupi ya jinsi mtambo unavyofanya kazi:  

 

Mtambo wa biogesi unatengeneza gesi (hewa ya ukaa) watu wanaweza kutumia kwa viti vingi. Mara nyingi watanzania wanatumia kwa kupikia chakula na biogesi au kutumia kwa kuwashia taa badala ya umeme. Mtambo wa biogesi unahitaji kinyesi tu kwa kutengeneza gesi. Mtambo wa biogesi una mashimo mawili. Ndani ya shimo la kwanza ndiko kinyesi kinawekwa ili kichachuke bila hewa ya oksiyen. Bakteria maalumu wanaweza kufanya kazi na hewa ya ukaa inatokea. Ndani ya shimo la pili kinyesi kinachachuka tayari kwa kutumika kama mbolea bila harafu mbaya na inaweza kufukuza wadudu. Kwa hivyo mtambo wa biogesi una faida nyingi. Unaboresha kinyesi kuwa mbolea bora na unapata gesi. Unaokoa hela ambayo ungetumia kununua mkaa na unatumia umeme angalau kidogo kuliko kabla ya kuanza kutumia biogesi.

 

Kwa maelezo zaidi: +255 713 334 584 (NRCF Korogwe)

 

Halafu tuliongea kwa muda mrefu kuhusu mtambo wa biogesi, kila mtu alitaka kuangalia mtambo wa biogesi. Kwa hivyo tuliondoka ofisini na tulienda kwa Mama Farida Mohamedi anaeishi Kilole na anafuga ng’ombe 4 na ufugaji wa wanyama ni sharti muhimu kwa kutumia biogesi. Tuliona vilima viwili na chombo kimoja tu. Ndani ya chombo anaweka kinyesi cha ng’ombe. Bomba linaanza hapa na kinyesi kinafika kwenye shimo la kwanza  la mtambo wa biogesi.

Hatukuweza kuangalia shimo hili, kwa sababu ni lazima bakteria wafanye kazi bila hewa. Lakini tuliweza kufungua shimo la pili. Na tuliona mbolea inapoelekezwa inapokua tayari. Bwana Madeni (biogas supervisior NRCF) alijibu maswali mengi. Halafu tulikwenda ndani ya jiko la Mama Farida. Tuliweza kuona jiko la kupikia na taa moja vinavyofanya  kazi kwa kutumia nishati ya biogesi. Lakini alisema hatumii taa. Anatumia biogesi kwa kupika tu, lakini kwa kupika inatosha kabisa. Hataji matumizi ya nishati ya  mkaa tena.  Na faida nyingine ni, kwamba kupika ni rahisi na haraka kwa kutumia nishati ya biogesi kuliko ya mkaa. Ametuambia anafuraha sana kutumia biogesi na tangu amejenga  mtambo wa biogesi hana tatizo lolote.

 

 

Halafu tuliendelea na safari. Tulipanda  gari tena na kwenda „Highway“. Ni sehemu kubwa kwani mabasi makubwa  ya abiria yanasimama hapo na abiria wanapumzika na kula chakula kisha wanaendelea na safari. Hapa wamejenga  mtambo wa biogesi mkubwa sana. Huu ni 26m3. Wanatumia kwa kupikia pia, lakini bado wanahitaji mkaa zaidi kwani mahitaji ya nishati kwa kupikia ni makubwa sana. Lakini biogesi inasaidia kupika na kupunguza matumizi ya mkaa. 

 

Mwisho tulienda kijijini ambaKo palikuwa na mkulima mkubwa. Analima mashamba mengi na makubwa. Anafuga  ng’ombe pia. Ana mtambo wa biogesi wenye ukubwa 13m3. Aliutengeneza mwaka 2013. Lakini hapa tuliona matatizo yanatokea mara kwa mara. Alisahau kuweka kinyesi ndani ya mtambo na alisahau kukoroga pia. Mkulima alituambia, hakutunza mtambo wa biogesi kwa karibu mwezi mzima. Bwana Madeni alisema kwa bahati mbaya anaona mtambo wa biogesi wenye matatizo ya aina hii mara kwa mara. Alisema ni tatizio kubwa watu wanaacha kutunza mtambo wa biogesi. Na kwa sababu nishati ya  biogesi haiachi haraka kama mtu anapoacha kuweka kinyesi ndani, watu hawaoni kwamba ni tatizo. Taratibu biogesi itakuwa ndogo, lakini athari si sasa hivi. Kwa hivyo watu wengine wanafikiri si shida kama hawatunzi mtambo wa biogesi kwa wiki moja au mbili. 

Tunatumaini mkulima ataanza tena kutumia biogesi. 

Baada ya kuangalia mitambo ya biogesi  mitatu, tulirudi ofisini na kuagana . Tukafikiri ni siku nzuri sana. Tulijifunza vingi sana. Alhamisi tuliendelea na safari!

 

Siku ya pili, 30.10.2014

 

Tulitukutana saa 4.00 Asubuhi na  wanafanyakazi 7 wa TALISDA na mmoja wa NRCF kwa kutembelea Lutindi. Lutindi Mental Hospital ilijenga mtambo wa biogesi  mwaka mmoja uliopita. Hospitali inafuga ng’ombe, kuku na nguruwe. Na wanahitaji mkaa mwingi sana, kwa sababu wanapika chakula kwa watu zaidi ya 200. Kwa hivyo kule ni sharti nzuri pia kwa kutumia biogesi. Kule tuliona mtambo wa biogesi umetunzwa vizuri. Ni mtambo wenye ukubwa wa 13m3, lakini bado hautoshi kabisa kupika kwa wote. Lakini hivi si shida, kwa sababau ni vizuri kuanza kutumia kidogo, kuliko kutokutumia kabisa. Gesi inasaidia na wanahitaji pesa ndogo kuliko kabla yake. Watu wanaoishi Hospitali wanafurahi sana kutumia biogesi. Wanatumia mbolea pia kwa mashamba yao. Na isitoshe tulijifunza, kwamba unaweza kutumia mbolea kama dawa pia. Wanyama wakiumwa kwa sababu  ya wadudu ndani ya matumbo yao, watu wanaweza kuongeza mbolea kidogo ndani ya chakula chao na kisha hao watakula na mbolea itafukuza wadudu. Na pia hospitali ilitengeneza bomba linaloanzia mwishoni mwa mtambo wa biogesi mpaka ziwa la samaki. Mbolea kidogo inaenda ndani kwenye ziwa na samaki wanaweza kula. Walitengeneza mtambo wa biogesi kwa ufanisi mkubwa.

 

Wanaziara walifurahi sana kutembelea. Safari  ilikuwa nzuri. Tuliangalia mlima, msitu na vijiji. 

Halafu siku ilikua ya kuvutia,  tulipanda gari na tulirudi ofisini NRCF. Pale tulifanya mazungumzo ya mwisho. Tuliuliza maswali ya mwisho na tulitoa mrejesho. Kwa ujumla ziara ilikua yenye mafunzo bora!

 

Tunashukuru tuliweza kwenda NRCF. Tunashukuru sana!

 

Idara ya maendeleo ya vijana na huduma za kujitolea:

 

Taasisi ya TALISDA ina idara ya watu wanaojitolea kufanya nao kazi mbalimbali, watu hao wanatoka Tanzania na nchi nyingine za kigeni. Wanashirikiana na wafanyakazi wa TALISDA katika shughuli mbalimbali kwa ajili ya kupata uzoefu wa kazi. Moja ya majukumu yao ni kushughulika na klabu za mazingira katika shule za sekondari kama vile shule ya sekondari ya kumbukumbu ya mwalimu Nyerere. Katika kushughulika na klabu hizi, vijana wanashirikiana na wanafunzi kutoa mbinu mbalimbli za kulinda mazingira kama vile kuepuka kukata miti ovyo, kutupa taka ngumu na momonyoko wa ardhi.

 

Zaidi ya hayo kuna program inayotekelezwa na idara hii hasa kwa vijana wazawa wanaojitolea. Mfano mradi wa WEKEZA (Wezesha ustawi Endeleza Kiwango cha Elimu Zuia Ajira kwa watoto) mkoa wa Tanga. WEKEZA ni mradi unayotekelezwa kwa ushirikiano na TALISDA Foundation kwa malengo ya kuendeleza elimu kwa watoto waliokwisha kuingia kwenye ajira au walio hatarini kuinigia kwenye ajira.

 

Katika mradi huu kijana mmoja hushirikiana na wafanyakazi wengine wa TALISDA pamoja na uongozi wa vijiji pamoja na kamati kutoa mafunzo kwa kamati za shule, wazazi, walimu pamoja na wafanyakazi wa serikali za vijiji husika katika wilaya za Korogwe, Muheza na Tanga. Mafunzo hayo ni kutoa elimu kuhusu namna ya kuandikisha WWKMH (Watoto Walio Katika Mazingira Hatarishi) walio katika ajira kwa watoto au kulinda watoto kuingia katika ajira za watoto. Pia wafanyakazi wa TALISDA na WEKEZA wanatoa elimu ya ujasiriamali kwa wazazi ili waweze kujiongezea kipato na hivyo kuzuia ajira kwa watoto.

bottom of page